Waziri wa zamani wa michezo wa Ivory Coast ambaye kwasasa ni mbunge, Alain Lobognan amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kusambaza taarifa za uongo kupitia ukarasa wake wa Twitter.

Januari 9, 2019 Lobognan aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa mkuu wa upelelezi ametoa amri ya kukamatwa kwa mbunge mwenzake, taarifa ambayo ilizua taharuki na fujo miongoni mwa wafuasi wake.

Aidha, baada ya tamko la mbunge huyo, mkuu wa upelelezi alijitokeza hadharani na kukanusha taarifa hizo zilizosambazwa na mbunge Labognan katika ukurasa wake wa Twitter.

Mbunge huyo ambaye kwa sasa yupo katika mgomo wa kula kwa siku ya kumi sasa amesema kuwa kesi yake imeingiliwa kisiasa, huku mwanasheria wake bi Affoussiata Bamba Lamine, amesema kuwa wana mpango wa kukata rufaa.

Pia, ameongeza kuwa kesi ya mteja wake imeingiliwa kisiasa, ambapo amesema kuwa mteja wake analengwa kwasababu ya ukaribu wake na waziri mkuu wa zamani ambaye alikua pia kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro.

Awali, mbunge huyo  alikuwa Spika wa Bunge la nchi hiyo, ambapo mwezi uliopita alitangaza kuachia madaraka kama. Wachambuzi wanasema kuwa huenda ameanza kujiandaa na kugombea urais mwaka 2020

LIVE BUNGENI: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Januari 31, 2019
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Januari 31, 2019