Bingwa wa masumbwi duniani kupitia uzani wa juu Tyson Luke Fury amekiri anatumia dawa za kulevya aina ya Cocaine kwa ajili ya kukabiliana na matatizo ya kiakili.

Bondia huyo raia wa nchini England amesema amekuwa akiugua ugonjwa wa akili kwa miaka kadhaa na hajafanya mazoezi tangu mwezi Mei.

Amesema amekua akilewa ulevi wa dawa hizo kwa siku za jumatatu hadi jumapili.

Fury ametoboa siri hiyo ikiwa ni baada ya siku mbili ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kukutwa umeandikwa taarifa za kustaafu kwake mchezo wa ndondi, lakini saa kadhaa baadae alikanusha kwa kusisitiza alikua akifanya utani.

Akizungumzia afya yake, Fury mwenye umri wa miaka 28 amesema hawezi kukabiliana na matatizo kuacha kuvuta dawa za kulevya kwani anapozitumia huepuka matatizo mengi ambayo huenda yakasababishwa na ugonjwa wa akili unaomkabili.

 

Video: Bodi ya wadhamini CUF yatua Mahakama Kuu
Video: Waziri Lukuvi awabana madalali, atoa masharti asema lazima yafuatwe