Bingwa wa ndodi wa uzani wa juu duniani Tyson Fury ametumia mitandao ya kijamii kutangaza kujiuzulu.

Raia huyo wa nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 28, alilazimika kujiondoa katika pambano la marudiao dhidi ya raia wa Ukraine Wladmir Klitschko, lililopangwa kufanyika Oktoba 29 kutokana na maswala ya kiafya.

Fury ambaye ni bingwa wa duniani kupitia WBA na WBO anakabiliwa na kesi mnamo mwezi Novemba inayohusisha madai ya utumiaji wa dawa za kusisimua misuli.

”Ndondi ni kitu kibaya zaidi nilichoshiriki”, umeeleza ukurasa wake wa mtandao wa Twitter: ”Mimi ndio bingwa, na aliyestaafu”

Fury alitarajiwa kupata kitita kikubwa tangu alipojiunga na ndondi wakati wa mpambano wake wa pili dhidi ya Klitschko katika uwanja wa Manchester mwezi huu.

Aliahirisha pambano la marudio dhidi ya raia huyo wa Ukraine, ambao ulipangwa kufanyika mwezi Julai baada ya kupata jereha la kifundo cha mguu wakati wa mazoezi.

Amepewa siku 10 na shirikisho la ndondi duniani WBO kutoa maelezo na kuahirishwa ka pambano hilo la marudio kwa mara ya pili.

Mario Balotelli: Simfahamu Jurgen Klopp
Gianni Infantino Apendekeza Timu 48 Kombe La Dunia