Bondia kutoka nchini England, Tyson Fury amevua fulana yake kuonyesha kitambi huku akimkandia mpinzani wake, Wladimir Klitschko kwa kujiruhusu kupigwa na ‘manyama uzembe’ kama yeye.

Kituko hicho alikifanya katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea pambano lao la marudiano la uzito wa juu litakalofanyika baadae mwaka huu.

Fury atatetea mataji yake ya dunia ya WBA na WBO aliyoyatwaa kwa kumshinda Klitschko mjini Dusseldorf, Ujerumani Novemba mwaka jana katika pambano litakalofanyika ukumbi wa Manchester Arena Julai 9.

“Mtu mnene – ambaye amekupiga wewe. Aibu yako,”alisema Fury akiwa amevua fulana huku akimgeukia Klitschko katika Mkutano na Waandishi wa Habari.

Fury also rubbished the notion that Klitschko would be able to transform his boxing style at the age of 40 in time for the contestTyson Fury akiwa na mpinzani wake Wladimir Klitschko katika picha ya pamoja wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

 

Arsene Wenger Kuifumua Safu Ya Kiungo Na Kuifuma Upya
Korea kuwapa Tanzania Walimu wa Hisabati na Sayansi kupunguza uhaba