Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limefunguka na kuweka wazi kuwa siku ya jana April 13, 2018 lilikutana na msanii Nandy kufuatia kuvuja kwa video yake akiwa faragha na msanii Bill Nas na kufanya naye mazungumzo.

BASATA wameweka wazi kuwa wamemtaka msanii huyo kuomba radhi Watanzania kwa kitendo hicho lakini pia baraza hilo limechukua jukumu la kuwakumbusha wasanii wengine juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii na kuwataka kutumia mitandao kwa lengo la kujiletea maendeleo.

“Baraza linawakumbusha na kuwaasa wasanii wote kutumia maendeleo ya teknolojia na mitandao ya kijamii kwa lengo la kujiletea maendeleo badala ya kutumia mitandao kusambaza vitu visivyo na manufaa kwao na vyenye kuwadhalilisha wao wenyewe, familia zao na umma kwa ujumla” amesema taarifa ya BASATA.

Hata hivyo msanii Nandy jana alipotoka Baraza la Sanaa la Taifa  (BASATA) aliweza kuandika maelezo marefu na kuomba radhi kwa Watanzania kwa kitendo cha video yake ya faragha kuvuja mtandaoni.

Merkel aunga mkono mashambulizi ya kijeshi nchini Syria
Kocha Mayanga atajwa kurithi mikoba nchini Kenya