Vijana siku hizi walio nje ya ndoa huishi maisha ambayo hufananishwa na maisha ya ndoa, kutembea pamoja, kula pamoja, kulala pamoja, kuzaa watoto na kuwaita majina pamoja, kulea pamoja, kucheza pamoja, kulia pamoja, kufurahi pamoja, kusafiri pamoja, kulipia gharama mbalimbali pamoja lakini  bado wanasema hawapo tayari kuoa na kuolewa.

Moja ya sababu ni uoga wa kuingia kwenye ndoa,  watu wengi hawana tafsiri nzuri ya maisha ya ndoa kutokana na waliyaona kwenye maisha ya ndoa ya ndugu, jamaa au marafiki zao ambayo yaliwakatisha tamaa ya kuoa au kuolewa.

Mwisho wa siku ikumbukwe kuwa kila mtu ana maisha yake, ulichopitia wewe sio atachopitia mtu mwingine alichopitia baba yako au mama yako au rafiki yako sio utachopitia wewe, kikubwa ni kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi, ni vyema kumjua mwenza wako vizuri kabla hujafanya maamuzi ya kuoa au kuolewa hii itakusaidia kuishi maisha ya furaha, amani na upendo ukiwa kwenye ndoa.

Kijana jifunze ndoa ni Baraka ya mambo yote unayoyafanya, hivyo kama mtu hana utayari wa kufunga ndoa na mototo wa watu basi ni vyema kuchukua maamuzi mapema kuepusha kupotezeana muda na malengo katika maisha usiwe mguu mmoja ndani mwingine nje.

Picha: Kilimanjaro Queens Yawasili Nchini Kupitia Kagera
Serengeti Boys Kwenda Rwanda Kesho

Comments

comments