Zaidi ya shilingi milioni 10 na viwanja 198 vya Shirika la Posta Tanzania vimebainika kuporwa na kumilikishwa kwa watu binafsi huku kukiwa hakuna maelezo yeyote.

Hayo yamesemwa na Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya TPC, Kanali Mstaafu Dkt. Haroun Kondo katika kikao cha viongozi waandamizi wa shirika hilo.

Amesema kuwa utapanywaji wa mali na fedha za shirika hilo uligunduliwa na Bodi hiyo mara baada ya kuteuliwa kazi yake ya kwanza ilikuwa ni kuhakiki mali na ukaguzi wa fedha za shirika.

Aidha, amesema wakati wa ukaguzi Bodi ilibaini kuwepo kwa akaunti 120 za shirika katika benki mbalimbali ambazo iliamua kuzifunga wakati ikiendelea na ukaguzi.

“Tulibaini matumizi ya fedha yalikuwa ya ovyo na shirika halikuwa hata na shilingi moja huku likiwa linadaiwa na wateja wake sh. 16 bilioni 16 huku watendaji wakiwa hawazifuatilii,”amesema Dkt. Kondo

Hata hivyo, akizungumzia mali za shirika hilo zilizopo mikoani amesema kuwa, baadhi ya viwanja vilishajengwa nyumba za watu binafsi na utaratibu wa kuvirudisha unafanyika.

 

Majaliwa aagiza Wakurugenzi wachunguzwe
Video: Vurugu kubwa zaibuka Kigamboni, Kivumbi Kinondoni na Siha