Ubalozi wa Uingereza nchini, umemtangaza  Diamond Platinumz kuwa balozi wa vijana wa Tanzania, kwa ajili ya mradi unaoangazia kutengeneza kizazi bora kijacho (next generation).

Uteuzi huo umetangazwa na Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose kupitia mtandao wa Twitter.

Ubalozi huo wa Diamond umeunganishwa na ushiriki wake katika mradi wa Next Generation Tanzania.

Kuna uwezekano mkubwa kuwa utendaji kazi wake, ukubwa na ushawishi wa Diamond hasa kwa vijana ni vigezo muhimu vilivyompa shavu hilo.

Waziri Mkuu Akabidhiwa Maabara ya Wananchi waishio vijijini
Picha: Roma, Kala Jeremiah wamtembelea Lowassa