Timu ya taifa ya Ubeligiji imefanikiwa kutokea nyuma kwa mabao 2 na kushinda kwa 3-2, mchezo wake wa raundi ya 16 bora dhidi ya Japan uliochezwa mjini Rostov Urusi na kuifikia rekodi ya Ureno ya mwaka 1966.

Ureno iliweka rekodi ya kutoka nyuma kwa mabao 2-0 na kushinda 5-3 ndani ya dakika 90 kama walivyofanya Ubeligji. Ureno yenyewe ikiwafunga Jamhuri ya Korea kwenye mechi ya robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966.

Mbali na rekodi hiyo ya Ureno, Ubeligji pia imevunja rekodi ya Ujerumani ya mwaka 1970 ambapo ilitoka nyuma kwa mabao 2 na kushinda dhidi ya England lakini wao wakishinda ndani ya dakika 120 lakini Ubeligji wameshinda ndani ya dakika 90.

Mabao ya Japan ambayo yaliwashangaza wengi yalifungwa kwa haraka haraka kipindi cha pili kupitia kwa Genki Haraguchi dakika ya 48 na Takashi Inui dakika ya 52. Ubeligji walisawazisha kupitia kwa Jan Vertonghen dakika ya 69 na Marouane Fellaini dakika ya 72 kabla ya Nacer Chadli kufunga bao la 3 dakika ya 90.

Hata hivyo, Ubeligiji sasa watakutana na mabingwa mara 5 wa Kombe la Dunia Brazil katika hatua ya robo fainali. Brazil waliwafunga Mexico mabao 2-0 kwenye mechi ya mapema.

Serikali ya Sudani yalaumiana na waasi wa nchi hiyo
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julia 3, 2018