Asilimis 80 ya wazazi na walezi wanaoishi mijini hawana muda wa kuzungumza na watoto wao, hali inayosababisha kuporomoka kwa maadili kwa watoto hao.

Meneja Mradi ‘Binti Jitambue’ Sara Akwisombe alizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam na kusema hali hiyo inasababishwa na wazazi kuwa na shughuli nyingi na kukosa muda wa kukaa na watoto wao.

Alisema hali hiyo pia ndio chanzo kikubwa cha mimba za utotoni kwani watoto hawana elimu ya uzazi kutokana na malezi waliyoyapata kutokidhi mahitaji yao.

”Wazazi wengi wamekuwa bize na shughuli zao za kila siku na kuwasahau watoto, jambo linalosababisha kuporomoka kwa maadili na watoto kujiamulia wanavyotaka bila kujali madhara, kampeni iliyofanywa na Asasi ya Dira ya vijana Tanzania (TYVA) Kwa Mkoa wa Dar es salaam wamebaini watoto wengi wamejiingiza katika mahusiano.

Kampeni iliyofanyika kwa takribani miezi 11 imeweza kuwafikia watoto  4,000 wenye miaka 10 hadi 16 na kuwaelimisha juu ya elimu ya afya ya uzazi makuzi na kujitambua,  na wamefanikiwa kwa kiasi kukubwa kuzungumza na wazazi na kuwaelimisha umuhimu wa kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao.

Pia Akwisombe aliiomba serikali na watu wenye nia njema na watoto kushirikiana katika mradi ‘Binti Jitambue’ ili kuwawezesha watoto kujitambua na kufanya maamuzi sahihi.

 

Nikki Mbishi: Nafsi ya Chidi Benz haiko tayari kusaidiwa kuacha Ngada
DC mjema: Wekeni mageti barabarani kudhibiti magari mazito