Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ametangaza mpango wa kuanzisha mradi mpya wa mtaa maalum wa vileo/vilevi vilivyokubalika kisheria, ikiwa ni siku moja tu baada ya mradi wa kuwasafirisha walimu bure kwa kutumia daladala kuanza kwa kuchechemea.

Akizungumza jana wilayani humo, Makonda alisema kuwa amepanga kuanzisha mtaa maalum wenye baa pekee katika wilaya yake ambapo wananchi wanaotaka kupata vileo hivyo wanaweza kufika katika mtaa huo.

“Kinondoni nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhiwa,” alisema. “Nasubiri muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na bar mpaka nyuma ya misikiti na nyuma ya makanisa,” aliongeza.

Makonda alisema kuwa huo ni muendelezo wa ubunifu wa miradi mbalimbali katika wilaya yake ikizingatiwa kuwa ndiyo wilaya yenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012. Kwa sasa inakadiriwa kuwa na watu kwasasa ikikadiriwa kufikia watu milioni 1.9.

Shaba Kuanza Na Hardrock Ligi Kuu Pemba
Lukuvi aahidiwa rushwa ya Bilioni 5