Serikali Mkoani Lindi imeazimia kuja na mbinu mahususi ambayo itasaidia kupunguza wimbi la utupaji taka katika fukwe zinazozunguka Manispaa hiyo.

Akizungumza na Dar24 Media Afisa Afya Manispaa ya Lindi, Seifu Abdallah Seifu amekiri kuwepo kwa taka ngumu katika fukwe ya bahari kuzunguka Manispaa hiyo zikiwemo chupa za maji na soda na mifuko laini ambavyo vinaathiri viumbe hai waishio Baharini .

Amesema kuwa wamefikiria kuja na mbinu ya kuweka vitunzio taka (dustbin) ili kutoa fursa kwa watumiaji na wafanyabiashara katika fukwe hizo ili kufanya mazingira rafiki kwa watumiaji wakiwemo wanaoenda kupumzika na kutalii.

“Ni azma ya Manispaa kuhakikisha kwamba kila sehemu kunakuwa na vitunzia taka na kipaumbele kwa sasa kitakuwa katika maeneo ya fukwe kwa ajili ya kurahisisha utupaji wa taka’’ Amesema Seifu

Aidha katika kutekeleza hilo amesema kumekuwa na changamoto ya watu kuhujumu miundombinu ikiwemo wizi wa vitunzia taka na kwenda kuvitumia kinyume na malengo mahususi ambayo yaliyowekwa na Manispaa.

Hata hivyo, amekiri kuwepo na changamoto ya baadhi wa wafanyabiashara wa chakula maarufu (Mama ntilie) wanaojisaidia pembezoni mwa fukwe hizo hali ambayo inatishia usalama wa afya zao na watumiaji wengine wa fukwe hizo huku baadhi ya Mama ntilie hao wakidai sababu inayopelekea hali hiyo ni ubovu wa choo hicho.

Majaliwa awaonya DC na DED, 'Jirekebisheni'
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 21, 2019

Comments

comments