Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi na uchafuzi wa mazingira ni janga la kidunia na kwamba Serikali inapaswa kuchukua hatua za kuhimili mabadiliko hayo na tabia za binaadamu, kwa kuweka mipango bora na mikakati thabiti.

Makamu Othman ameyasema hayo akiwa Bumbwini Kaskazi B na Dunga Wilaya ya Kati Unguja, wakati alipokuwa akizungunza na viongozi wa Mikoa, Wilaya, Halmashauri, Mabaraza ya Miji, Masheha na Watendaji mbali kuhusu Mpango wa Serikali wa Kurithisha Zanzibar kuwa ya Kijani.

Baadhi ya masheha, madiwani na watendaji wa Ofisi za wilaya, Halmashauri na Mkoa wa Kaskazini Unguja wakimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais Othman Masoud Othman ( haytupo pichani) katika Ukumbi wa Skuli ya Bumbwini wilaya ya Kaskazini B Unguja leo kuzungunza na watendaji hao kuhusu mpango wa serikali wa kuirithisha Zanzibar kuwa ya kijani.

Amesema, kutokana na athari hizo hivi sasa sehemu kadhaa za viswa vya Zanzibar zinaendelea kuathirika kwa maji ya chumvi kupanda na kuingia katika mashamba ya wakulima na mengine kukimbilia sehemu za makaazi ya watu, huku kukiwepo mmongonyoko mkubwa wa fukwe, jambo linalotishia kuwepo janga kubwa la kimazingira hapa Zanzibar.

Hata hivyo, Othman amefahamisha kuwa kutokana na hali hiyo, Serikali iumekuja na mpango Jumuishi wa kuirejesha Zanzibar kuwa ya kijani kwa kuwashajiisha wananchi kujenga utamaduni kupanda miti na kuitunza, kuanzia ngazi utotoni ili kuisaidia nchi kuepukana na janga hilo.

Viongozi pambaneni ukatili wa kijinsia, watoto: Dkt. Gwajima
Tanzania, Norway kushirikiana miradi uhifadhi wa Mazingira