Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi jimbo la Pandani Pemba kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Profesa Omar Fakih Hamad ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi huo mdogo.

Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) imemtangaza Profesa Hamad kuwa mshindi kwa kupata kura 2,361 dhidi ya Mohammed Juma wa Chama cha Mapinduzi (CCM) aliyepata kura 1,934.

Tume iliendesha uchaguzi huo jana, Machi 28, 2021 baada ya aliyekuwa mwakilishi wa jimbo hilo, Aboubakar Khamis wa ACT Wazalendo kufariki dunia Novemba, 2020.

Uchaguzi huo ulihusisha vyama kumi vya siasa, ambavyo ni CCM, UPDP, ACT-Wazalendo, CUF, Ada Tadea, AAFP, ADC, NRA, NLD na Demokrasia Makini.

Katika hatua nyingine, Mgombea wa udiwani wa Wadi ya Kinuni, Unguja kwa tiketi ya CCM, Maryam Rajab Masinga ameshinda kwa kishindo uchaguzi mdogo wa wadi hiyo, akipata kura 2,376 (sawa na asilimia 87.6). Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa na ZEC, Bi. Rajab mshindani wake wa karibu zaidi Hamad Hassan Hamad aliyepata kura 313.

KISHINDO CHA RAIS SAMIA: Marais wanawake yalivyoishangaza dunia (video)
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 29, 2021