Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imetangaza kuahirisha uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika Jumapili ya wiki hii na kusogeza wiki moja mbele.

Uchaguzi huo kwasasa umepangiwa kufanyika Jumapili tarehe 30 Disemba badala ya tarehe 23 iliyokuwa imepangwa uchaguzi kufanyika mwaka huu.

Tume hiyo imesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuchelewa kwa shughuli mbalimbali za kufikisha vifaa na mitambo ya kupigia kura katika maeneo ya vituo

Aidha, uchaguzi wa nchini Congo DRC umekuwa ukisogezwa mbele kwa zaidi ya miaka miwili sasa, huku rais anayemaliza muda wake, Joseph Kabila akituhumiwa kwa kutoa visingizio kadhaa vya kuahirisha uchaguzi ili aendelee kubaki madarakani.

Hata hivyo, hivi karibuni jengo la tume ya uchaguzi nchini humo liliteketea kwa moto, lakini tume hiyo imewahakikishia wananchi kuwa moto huo hautaathiri kufanyika kwa uchaguzi.

Video: Makonda anusurika mtego wa JPM ''Makonda bahati yako sana,''
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Desemba 21, 2018

Comments

comments