Matokeo rasmi ya uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya Jumanne hayajatangazwa na tume ya uchaguzi ya Malawi, lakini chombo cha habari cha serikali MBC kinasema kwamba kiongozi wa upinzani Lazarus Chakwera anaongoza na asilimia 59 ya kura zilizohesabiwa.

Rais Peter Mutharika , ambaye anawania muhula wa pili ana asilimia 38 ya kura zilizohesabiwa, Mgombea wa tatu ambaye hakuonekana kama mgombea mkuu, anasemekana kujiapatia asilimia 2 ya kura hizo.

Mwaka uliopita, Malawi ilikuwa nchi ya pili barani Afrika kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais kufuatia madai ya udanganyifu, baada ya Kenya 2017.

Wafuasi wa bwana Chakwera tayari wameanza kusherehekea kile wanachoamini ni ushindi wa kihistoria – katika kile kinachoaminika kuwa tukio la kwanza katika eneo la sahara kwamba uchaguzi uliokumbwa na udanganyifu umebadilishwa na upinzani kuibuka na ushindi ukichukua madaraka kwa njia ya kidemokrasia.

Eymael afichua kinachoisumbua Young Africans
Mchakato wa Rais Putin kusalia hadi 2036 washika kasi