Wanaanchi wa Siera Leone wamelazimiaka kurudia uchaguzi ili kuchagua raisi mpya wa nchi hiyo kufuatia raisi aliye shinda uchaguzi uliofanyika machi 7, kushindwa kufikisha asilimia 55 ya kura zilizopigwa.

Kwa mujibu wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo ,Uchaguzi umepangwa kurudiwa tena machi 27 mwaka huu.

Aidha,katika uchaguzi uliofanyika awali chama kikuu cha upinzani nchini humo cha Peoples Party (SLPP) kinacho ongozwa na Julius Maada kilishinda kwa kura milioni 1.1 sawa na asilimia 43, kikifuatiwa na chama tawala cha All Peoples Congress (APC) kinachoongozwa na Samura Kamara, aliyepata asilimia 42 ya kura zote zilizopigwa.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi nchini humo raisi anatakiawa kuchaguliwa kwa zaidi ya asilimia 55 ya kura zote zilizopigwa, hivyo wagombea hao wote walishindwa kufikia asilimia hiyo.

Hata hivyo, Julius Maada, ambaye aliongoza uchaguzi wa awali anawania nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya kushindwa kwenye uchaguzi wa 2011 dhidi ya raisi aliye maliza muda wake, Ernest Bai Koroma wakati mpinzani wake mkubwa Samura Kamara alikuwa waziri wa mambo ya nje kabla ya kuamua kuwania nafasi hiyo ya urais nchini siera Leone.

Mradi bomba la mafuta Hoima kugawa ajira 10,000 kwa watanzania
Viongozi Mtandao wa Wanafunzi waitwa kwa DCI kesi ya Nondo