Raia wa Gabon wanapiga kura ili kuweza kuchagua rais wao,wagombea wa uchaguzi huo ni rais aliyeko madarakani Ali Bongo, na mpinzani wake mkuu, Jean Ping, ambaye alikuwa kiongozi wa zamani wa tume ya umoja wa Afrika.

Rais Bongo alichukua wadhifa wa urais mwaka 2009 baada ya kifo cha babake Omar Bongo.

Rais Bongo anapewa  nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo, kwani anadhibiti serikali na mshindi anahitaji kumzidi mpinzani wake kwa kura moja pekee.

Hata hivyo upinzani umelezea wasiwasi kwamba serikali tayari ‘imetayarisha matokeo yake.

Ijumaa iliyopita katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon alitoa wito kwa pande zote mbili kudumisha amani kabla na baada ya uchaguzi huo,wagombea kumi ndio pekee wanaowania kiti hicho cha urais.

Katika kampeni za uchaguzi huo, chama cha rais Ali Bongo Gabonese Democratic Party (GDP) kimekuwa kikiwapa watu zawadi, zikiwemo simu, jokofu na mashine za kufua nguo na mshindi wa uchaguzi huo, ataongoza kwa muhula wa miaka saba.

Gabon ni miongoni mwa wazalishaji wakuu wa mafuta barani Afrika, japo theluthi ya raia wake ni maskini na inaidadi ya raia milioni 1.5 pekee

Prof.Muhongo Awapa Neno Wanafunzi Waliopata Ufadhili Wa Masomo Ya Mafuta Na Gesi
Bunge la Tunisia laidhinisha serikali ya Youssef Chahed