Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha soka Mkoa wa Pwani (COREFA), kwa mara nyingine imeusimamisha uchaguzi wa Chama cha Soka Wilaya ya Bagamoyo (BFA) uliokuwa ufanyike kesho July 30, 2016.

Kusimamishwa kwa uchaguzi huo ni kutokana na mapingamizi kutoka kwa baadhi ya wagombea wakipinga mfumo mzima wa usaili uliofanyika jana na kuwahalalisha wagombea wote kuingia katika kinyang’anyilo wakati miongoni mwao wakiwa hawana sifa za kuwa wagombea.

Hussein Kipindula ni mmoja wa wagombea anayeomba kugombea nafasi ya Katibu wa BFA ambaye amewasilisha katika Kamati yangu pingamizi la kupinga baadhi ya wagombea kuruhusiwa kugombea nafasi walizoziomba wakati hawana sifa.

Katiba ya BFA ibara ya 29 (2) inaeleza sifa ya Elimu ya kuanzia kidato cha nne anayotakiwa kuwanayo yeyote anayetaka kugombea na kuchaguliwa kuwa kiongozi wa BFA, sifa ambayo Bw. Kipindula amesema wagombea baadhi hawana lakini wameruhusiwa kugombea!

Ili kuondoa mkanganyiko huo, Kamati yangu imeamua kuusimamisha uchaguzi huo, ili usaili uanze upya na kuiagiza Kamati ya Uchaguzi ya Wilaya ya Bagamoyo (BFA) kuleta kwa Kamati yangu nakala ya vyeti vya elimu vya wagombea vikaakikiwe Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Ni matumaini yangu kwamba, maelekezo na maagizo ya Kamati yangu kwa Kamati ya Uchaguzi Bagamoyo (BFA) yatatekelezwa kwa haraka ili BFA iwapate viongozi wenye sifa kwa mjibu wa Katiba na Kanuni za uchaguzi za TFF na wagombea wote watatoa ushirikiano wa kutosha katika kuondoa mkanganyiko huo.

Imeandaliwa na;
Masau Bwire
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi Mkoa wa Pwani (COREFA)

Video: Jambazi hatari auawa, Akutwa na bastola aina ya Glock17 na risasi sita
TRL Yafanya Mabadiliko Safari Za Treni