Kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF) imetangaza uchaguzi mkuu wa klabu ya Young Africans kuwa utafanyika Juni 25, 2016 badala ya Juni 5, 2016.

Kamati ya uchaguzi ya TFF imelazimika kufanya hivyo kwa kuzingatia ushiriki wa Young Africans ambayo inashiriki michuano ya kimataifa.

Sekretarieti ya Young Africans ambayo ingefanya kazi kwa pamoja na kamati ya uchaguzi kwa kushirikiana na TFF kwa sasa inashughulikia pia kuiandaa timu kwa ajili ya michuano ya kimataifa.

Young Africans inatarajiwa kucheza na Esperanca ya Angola katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika Mei 7, mwaka huu kabla ya kurudiana kati ya Mei 17 na 18, mwaka huu huko Angola.

Katiba itakayotumika katika uchaguzi huo ni ya mwaka 2010 na kwamba wanachama wa Young Africans watatumia kadi za kawaida za uanachama na si za benki.

Simba Yarejea Kisiwani Unguja Kupanga Mikakati Ya Jumapili
Magufuli akubali Kuyabeba mazito ya Kikwete