Jana, Zanzibar ilifanya uchaguzi wa marejeo kama ilivyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), pamoja na jimbo moja la Kijitoupele ambalo halikufanya uchaguzi Oktoba 25 mwaka jana.

Matokeo ya awali ya uchaguzi huo katika baadhi ya majimbo yameanza kutangazwa ambapo CCM imeendelea kuongoza kwa tofauti kubwa.

Majimbo mawili tayari yameshapata Wawakilishi ambayo ni Kijitoupele na Ziwani.

Katika Jimbo la Kijitoupele, Nahodha Shamsi Vuai (CCM) ametangazwa mshindi wa Ubunge Jimbo la Kijitoupele kwa kupata kura 12,473 akimuacha kwa mbali Mohamed Juma wa CUF ambaye amepata kura 202.

Wengine, ni Zaituni ally Khamis ACT kura 155, Salim Ally Omar CCK kura 73, Demokrasia Makini amepata kura 67, UPDP kura 79.

Katika Jimbo la Ziwani eneo la Madungu, CCM pia imeshinda kwa tofauti kubwa ya kura ambapo mgombea wake Suleiman Makame Ali amepata kura 2,789 akifuatiwa na mgombea wa ADC aliyepata kura 381, UPDP 221 na Moh’d Ali Salum (CUF)aliyepata kura 153.

Katika majimbo mengine, matokeo yanaonesha kuwa Jimbo la Chakechake aliyeshinda ni Suleiman Said wa CCM, Jimbo la Ole mshindi ni Musa Ali Musa wa CCM, Jimbo la Wawi mshindi ni Hamad Ali Rashid wa CCM, Jimbo la Ziwani mshindi ni Asaa Ali Hamad wa UPDP, Jimbo la Chonga mshindi ni Shaibu Ali wa CCM.

Hata hivyo, CUF walitangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo licha ya majina ya wagombea wao kuorodheshwa na kupigiwa kura.

 

Djokovic Achuana Na Rafael Nadal Kuweka Rekodi Ya Masters Crown
Louis van Gaal: Rashford Ni Shujaa Wa Man Utd