Kupitia takwimu mpya zilizochapishwa hii leo Novemba 11, 2022 zinaonesha uchumi wa Uingereza ulianguka kwa asilimia 0.2 katika robo ya tatu ya mwaka 2022 hali inayothibitisha kuwa taifa hilo limetumbukia kwenye mdodoro wa kiuchumi.

Hatua hii inakuja ikiwa ni wiki moja tangu Benki Kuu ya nchi hiyo kutoa hadhari kwamba uchumi wa Uingereza unaelekea kudorora katika wakati umma unapambana na kupanda kwa gharama za maisha na mfumuko wa bei wa kiwango cha juu.

Ujumbe wa Wananchi kupitia mabango nchini Uingereza. Picha ya ZUMAPRESS

Waziri wa fedha wa Uingereza, Jeremy Hunt amesema takwimu hizo mpya zinaashiria hali itazidi kuwa ngumu na serikali ya nchi hiyo italazimika kuchukua maamuzi magumu kurejesha utulivu wa kiuchumi.

Hata hivyo, Serikali ya Waziri Mkuu, Rishi Sunak inatazamiwa kutangaza bajeti mpya ambayo kiongozi huyo anatumia itasaidia kuleta uthabiti wa kisiasa na kiuchumi baada ya mtikisiko wa wiki za karibuni ndani ya utawala wa taifa hilo mapema wiki ijayo.

Taasisi 455 zatumia mfumo mpya wa taarifa
Samia aridhia Wanafunzi kuendelea na usajili