Kampuni inayotoa huduma za usafiri jijini Dar es salaam UDART, imesitisha huduma zake kutokana na kufungwa kwa barabara ya Morogoro kutokana na daraja la mto Msimbazi kufunikwa na maji.

Katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Deus Bugaywa amesema kuwa huduma hiyo imesitishwa mpaka pale hali itakapotengemaa na kurudi katika hali yake ya kawaida.

“Tunasitisha kutoa huduma ya usafiri kwasasa, sababu kubwa ni za kiusalama, pale katika daraja la mto Msimbazi limefunikwa na maji hivyo mabasi hayawezi kupita, huduma hii itarejea pindi tu hali itakapokuwa shwari,”amesema Bugaywa

Madaraja jijini Dar yasombwa na maji
Mafuriko yasababisha kufungwa kwa barabara jijini Dar