Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimemtunuku Shahada Ya Heshima ya Sheria Ya Udaktari, rais Jakaya Mrisho kikwete katika mahafali ya 41 ya chuo hicho yaliyofanyika jana (Julai 21, 2015).

Kabla ya kumkabithi cheti na kumvisha joho, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Taaluma, Profesa Florens Luoga, alisema uamuzi wa kumtunukia shahada hiyo ya juu ulifanywa na seneti kwa umakini mkubwa na kuridhiwa na Baraza la Chuo Kikuu hicho.

“Seneti Ilizingatia husara, wema na umakini uliodhihirika katika maisha yako yote ya uongozi, tangu ulipokuwa kijana hadi ulipofikia ngazi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu,” alisema Prof. Luoga.

Baada ya kukabithiwa cheti hicho , rais Kikwete aliushukuru uongozi wa chuo hicho na kuahidi kuendelea kukisaidia chuo hicho.

“Nitaendelea kutoa mchango katika chuo chetu ambacho ndio chuo kikubwa hapa nchini, kwa lolote ambalo naweza kulifanya kwa ajili ya chuo sasa na hata baadae,” Rais Kikwete alisema.

Aliyemmwagia Fedha Bandia Blatter Kukiona Cha Moto
Arturo Vidal Kuitosa Juventus