Kufuatia ajali ya gari iliyotokea June 11, 2018 majira ya saa tatu usiku eneo la Ubungo, Riverside na kusababisha vifo vya wanafunzi wawili wa Chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM), Maria Godian Soko (Mwaka wa kwanza COSS) na Steven E Sango  (CPE CoET mwaka wa pili) na dereva mmoja .

Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM), umetoa taarifa ya kukatisha ratiba ya masomo kwa muda wa masaa matatu kuanzia Saa 4:00 asubuhi hadi Saa 7:00 mchana kesho Juni 14, 2018  ili kutenga muda wa kuaga miili ya waliokuwa wanafunzi na watumishi wa chuo hicho.

Taarifa hiyo imetolewa leo Juni 13, 2018 na Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma Profesa Bonaventure Rutinwa.

Taratibu za kuaga miili ya marehemu zitafanyika katika ukumbi wa Nkurumah uliopo chuoni hapo siku ya kesho Juni 14, 2018 kuanzia Saa 4:00 Asubuhi.

Endelea kufuatilia Dar24 kupata taarifa kwa kila litakalojiri katika safari ya mwisho ya wanafunzi waliokufa katika ajali ya gari iliyotokea aneo la Ubungo Riverside na kupoteza wanafunzi wawili.

 

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 14, 2018
Christian Bella, Walid kupamba tamasha la 'Seafood Gala 2018'

Comments

comments