Fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Barani Ulaya inatarajiwa kuchezwa Jumamosi hii kati ya timu za Real Madrid ya Hispania na Liverpool kutoka Uingereza ambazo zimefunga mabao mengi zaidi msimu huu huku washambuliaji bora zaidi duniani wakikutana.

Real Madrid wanatafuta ushindi wa 13 na wa tatu mfululizo huku Liverpool wakitaka kuingia katika orodha ya vilabu vilivyopata ushindi mara nyingi zaidi katika mashindano hayo makubwa barani humo endapo wataibuka washindi huko Kiev nchini Ukrine.

Aidha, timu hizo zinakutana zikiwa zimefunga zaidi ya mabao 90 kwenye mashindano yote msimu huu hivyo ni wazi kuwa fainali ya leo itakuwa kama vita kati ya Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na Mohamed Salah wa Liverpool.

Cristiano Ronaldo na Mohamed Salah wote wako mbioni kushindania tuzo ya Ballon d’Or mwishoni mwa mwaka huu 2018.

Hata hivyo, mwanzoni mwa msimu huu kulikuwa na mashaka kuhusu safu ya ulinzi ya Liverpool, lakini kufuatia kurejea kwa Virgil van Dijk mwezi Januari na kuimarika kwa kipa, Loris Karius wameongeza nguvu katika safu.

 

JPM atoa shavu jingine Bima (TIRA)
Video: Magufuli, Mkapa, Mangula siri nzito, DC amsweka ndani mwenyekiti CCM