Shirikisho la Soka Barani Ulaya UEFA limekataa ombi la nchi ya Ujerumani kutumia taa zenye rangi za ‘UPINDE WA MVUA’ kama urembo wa uwanja wa Allianze Arena ambao utatumika kwenye mchezo wa mwisho wa kundi F dhidi ya Hungary, kesho Jumatano (Juni 23).

Ujerumani iliwasilisha ombi hilo UEFA, ili kuiunga mkono Serikali ya Hungary ambayo inakubali vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja.
Rangi za ‘UPINDE WA MVUA’ hutumika kwenye bendera za chama cha Mashoga duniani, na Ujerumani waliamini kufanya hivyo ingeonesha dunia ni vipi wanavyoungana na Serikali ya Hungary kupitia mchezo wao wa kesho Jumatano (Juni 23).

“Kwa kuzingatia muktadha wa kisiasa wa ombi hili maalum – ujumbe unaolenga uamuzi uliochukuliwa na bunge la kitaifa la Hungary – UEFA lazima ikataze ombi hili.” Imeeleza taarifa ya UEFA.

Tayari Nahodha na Mlinda Mlango wa Ujerumani amejikuta matatani, na anaendelea kuchunguzwa na UEFA, kufuatia kuvaa kitambaa cha unahodha ambacho kilikua na rangi za ‘UPUNDE WA MVUA’ wakati wa mchezo wa dhidi ya Ureno mwishoni mwa juma lililopita.

Hivi karibuni nchi ya Hungary ilipitisha sheria ambayo ingezua taharuki miongoni mwa wanasiasa Barani Ulaya ambao wameanza kutafsiri nchi hiyo ina nia ya kukuza na kuendeleza ushoga na mabadiliko ya jinsia.

Nchi hiyo, inayoongozwa na Victor Orban, inachukuliwa kama ya kidemokrasia kidogo kuliko wenzao wengi wa Umoja wa Ulaya na iko chini ya shinikizo kwa rekodi yake ya haki za binadamu.

Kikosi cha Ujerumani kitaingia Uwanjani hiyo kesho, huku kikihitaji ushindi dhidi ya Hungary ambao utawahakikishia nafasi ya kutinga hatua ya 16 Bora.

Hungary nayo itahitaji ushindi dhidi ya wenyeji wao, ili kufikisha alama 4, ambazo zitaweza kuwavusha kutoka hatua ya Makundi hadi hatua ya 16 Bora.

Manji kushiriki mkutano mkuu Young Africans
Azam FC: Namungo FC walizijua mbinu zetu