Klabu za Arsenal, Chelsea na Manchester City zitafahamu wapinzani wao katika hatua ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya hivi leo.
Manchester United ndiyo timu pekee kutoka Uingereza ambayo haikufuzu kwa hatua hiyo ya muondoano na watakuwa wakisubiri kufahamu wapinzani wao katika Europa League.
Droo ya kupanga mechi za raundi ya muondoano itafanyika Nyon, Uswisi. Hafla itaanza saa 11:00 GMT ambazo ni sawa na saa nane saa za Afrika Mashariki.
Katika droo hiyo kuna vyungu viwili na cha kwanza ni kile cha washindi wa makundi ambao watapangwa na mpinzani kutoka chungu cha pili cha timu zilizoshika nafasi ya pili kwenye makundi yao.
Kwa mujibu wa kanuni za Uefa klabu kutoka nchi moja na zile zilizokuwa kundi moja haziwezi kupangwa pamoja.
Wakati huo huo Uefa itapanga ratiba ya michuano ya Europa League, michuano ambayo inashirikisha timu 32 huku timu 8 zikiwa ni zile ziliondolewa katika michuano ya klabu bingwa kwa kushika nafasi ya tatu kila kundi.
Timu 8 zilizotoka katika klabu bingwa ni Man United, Bayer Leverkusen, Olympiakos, Porto, Shakhtar Donetsk, Galatasaray, Sevilla na Valencia.
Mambo yalivyokuwa kwenye makundi UEFA:
Kundi A
Zilizofuzu: Real Madrid, Paris St-Germain
Europa League: Shakhtar Donetsk
Zilizoondolewa: Malmo
Kundi B
Zilizofuzu: Wolfsburg, PSV Eindhoven
Europa League: Manchester United
Zilizoondolewa: CSKA Moscow
Kundi C
Zilizofuzu: Benfica, Atletico Madrid
Europa League: Galatasaray
Zilizoondolewa: Astana
Kundi D
Zilizofuzu: Manchester City, Juventus
Europa League: Sevilla
Zilizoondolewa: Borussia Monchengladbach
Kundi E
Zilizofuzu: Barcelona, Roma
Europa League: Bayer Leverkusen
Zilizoondolewa: BATE Borisov
Kundi F
Zilizofuzu: Bayern Munich, Arsenal
Europa League: Olympiakos
Zilizoondolewa: Dinamo Zagreb
Kundi G
Zilizofuzu: Chelsea, Dynamo Kiev
Europa League: Porto
Zilizoondolewa: Maccabi Tel Aviv
Kundi H
Zilizofuzu: Zenit St Petersburg, Gent
Europa League: Valencia
Zilizoondolewa: Lyon