Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) limedhamiria kufanya mabadiliko ya kanuni za michuano ya ligi ya mabingwa barani humo, kwa kupendekeza ushiriki wa moja kwa moja kwa klabu ambazo zitamaliza kwenye nafasi nne za juu katika misimamo ya nchi ambazo zitakua na sifa hiyo.

Mabadiliko hayo yatazihusu nchi za England, Ujerumani, Hispania, pamoja na Italia.

Kamati ya mashindano ya UEFA imependekeza kanuni hiyo ili iweze kufanyiwa mabadiliko katika mkutano mkuu wa wajumbe wa shirikisho la soka barani Ulaya.

Hata hivyo kamati hiyo imesisitiza kuwa, itapendeza kanuni hiyo ikafanya kazi kati ya mwaka 2018-2021 kwa majaribio ili kuona kama itakua na mashiko yanayokusudiwa.

Sababu kubwa ya kamati hiyo kupendeza suala hilo, ni baada ya kufanya uchunguzi wa kina na kuibaini klabu ambazo zimekua zikimaliza katika nafasi ya nne zimekua zikishindwa kuitumia vyema bahati hiyo, hasa pale inapojitokeza wanapotolewa kwenye michezo ya mchujo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mapendekezo hayo yanatarajiwa kuwasilishwa katika mkutano mkuu ambao utakua na agenda ya uchaguzi wa kuziba nafasi ya rais wa UEFA aliyejiuzulu kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za FIFA Michel Platini, uliopangwa kufanyika Septemba 14-15, mjini Nyon nchini Uswiz.

Video: TRA imeuleta mfumo kuhakiki, kuboresha taarifa za mlipa kodi
Rais Aliyeupa Heshima Mchezo Wa Soka (Joao Havelange) Afariki Dunia