Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA), limewatoa hofu mashabiki watakaokwenda katika fainali za mataifa ya barani humo (Euro 2016), kwa kusema hali ya kiusalama itaimarishwa nchini Ufaransa zitakapofanyikia fainali hizo.

UEFA, wametoa tamko hilo kufuatia hofu iliyotanda miongoni mwa mashabiki wa soka walioweka dhamira ya kwenda nchini Ufaransa, baada ya matukio ya kigaidi yalilotokea jana katika mji wa Brussels nchini Ubelgiji.

Watu 34 wameripotiwa kupoteza maisha katika matukio hayo ambayo yaliyokea katika uwanja wa ndege wa Zaventem pamoja na kituo cha treni cha Maalbeek Metro.

UEFA, wamesisitiza kwamba kabla ya kutokea matukio hayo, tayari walikua wameshahakikishiwa na serikali ya nchini Ufaransa juu ya usalama wa mashabiki watakaokwenda nchini humo, ambapo inadaiwa kila hatua itakua chini ya uangalizi mkali.

Fainali za mataifa ya barani Ulaya zimepangwa kuanza kuunguruma kuanzia Juni 10 hadi Julai 10 mwaka huu, katika miji ya Saint-Denism, Marseille, Lyon, Lille, Bordeaux, Paris, Saint-Étienne, Nice, Lens pamoja na Toulouse.

Mataifa yatakayoshiriki fainali hizo ni Albania, Austria, Belgium, Croatia, Jamuhuri ya Czech, England, France, Germany, Hungary, Iceland, Italy, Ireland ya kaskazini,Poland, Ureno, Jamuhuri ya Ireland, Romania, Russia,Slovakia, Spain, Sweden,  Switzerland, Turkey, Ukraine pamoja na Wales.

Wekundu Wa Msimbazi Na Hadithi Za Kususia Michezo Ya Ligi
Andy Murray Ampinga Novak Djokovic