Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeipiga faini klabu ya Man City ya England kiasi cha Euro 3000 sawa na shilingi za Tanzania milioni 7.6 kwa kosa la kuvaa jezi za mazoezi zinazokiuka sheria.

Man City walifanya kosa hilo mwezi uliopita wakati kikosi chao kilipokua kinapasha misuli moto, kabla ya kuanza kwa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid.

Wachezaji wa Man City walivaa jezi zenye logo ya mdhamini ambayo ilikuwa kubwa zaidi na kukiuka sheria za michuano hiyo.

Kwa kawaida kuna kiwango cha ukubwa wa Logo inayotakiwa kukaa kwenye jezi lakini Man City waliweka kubwa, UEFA wamewapa Man City siku 90 za kukata rufaa kama wataona wameonewa, mchezo huo wa 16 bora ulimalizika Man City ikishinda 2-1.

Sheria za UEFA zinaeleza kuwa ukubwa wa logo ya mdhamini katika jezi za kupashia misuli joto kabla ya mchezo au makoti wanayoingia nayo dakika chache kabla ya mchezo kuanza yanapaswa kuwa na saizi ya Sentimita za mraba 20 na Sentimita za mraba 200 kwa sare nyingine zisizokuwa za kuchezea.

Wananchi Mauritius kununua bidhaa kwa Alphabet
Mtwara ruksa kunywa gongo ya mabibo