klabu ya Real Madrid itapambana na mahasimu wao wa mji wa Madrid Atletico Madrid, katika hatua ya nusu fainali huku mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC wakipangwa kukutana na AS Monaco.

Mahasimu hao wanakutanishwa katika michuano hiyo ikiwa ni mara ya tatu ndani ya miaka minne, kwani waliwahi kukutana kwenye michezo ya hatua ya fainali msimu wa 2013/14 na 2015/16.

Katika michezo hiyo Real Madrid walifanikiwa kuwafunga Atletico Madrid na kutwaa ubingwa wa barani.

Ratiba ya michezo hiyo imefahamika baada ya maafisa wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kuchezesha droo mchana huu katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho hilo huko mjini Nyon nchini Uswiz.

Washindi wa michezo hiyo watacheza hatua ya fainali katika mji wa Cardiff nchini Wales mwezi ujao.

Michezo ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali itachezwa Mei 2 na 3, huku michezo ya mkondo wa pili ikipangiwa Mei 9 na 10.

Young Africans, Tanzania Prisons Kumalizia Robo Fainali ASFC
Mpina aagiza watendaji wa taasisi kutoa taarifa za mazingira