Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, muda machache uliopita limekamilisha hatua ya upangaji wa ratiba ya michezo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya ambayo inaingia katika hatua ya robo fainali.

Shughuli ya upangaji wa ratiba ya hatua ya robo fainali, imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA uliopo mjini Nyon nchini Uswiz, kwa kuwashirikisha maafisa wa klabu zote nane ambazo zilifanikiwa kupenya katika mshike mshike wa michezo ya hatua ya 16 bora.

Ratiba inaonyesha kwamba wawakilishi pekee wa nchini England katika michuano hiyo Man City wamekabidhiwa mabingwa wa soka nchini Ufaransa Paris Saint-Germain.

Mabingwa wa kihistoria katika mchezo huo Real Madrid wao wamepangwa kukutana na wawakilishi wa Ujerumani VfL Wolfsburg ambao wataanzia nyumbani na kisha kuelekea nchini Hispania kucheza mchezo wa mkondo wa pili.

FC Bayern Munich wao wamepangwa kukutana na Benfica, huku mabingwa watetezi FC Barcelona wakikutana na Atletico Madrid.

Ratiba kamili ipo kama ifuatavyo.

Barcelona Vs Atletico Madrid

Bayern Munich Vs Benfica

Paris Saint Germain Vs Manchester City

Wolfsburg Vs Real Madrid

Michezo ya hatua ya robo fainali imepangwa kuchezwa April 05 na 06 na kurejewa Aprik 12 na 13.

TFF Yatoa Baraka Kwa Young Africans, Azam FC
Twiga Stars Kuwafuata Wazimbabwe Leo