Siku moja baada ya kusambaa habari kwenye mitandao ya kijamii na tovuti kadhaa kuwa hotel ya Kitalii ya Serena imefungwa kwa madai ya kubainika kukwepa kodi, uongozi wa hotel hiyo umekanusha taarifa hizo.

Taarifa hizo zilizosambazwa zilieleza kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imechukua uamuzi wa kuifunga hotel hiyo baada ya kubaini kuwa ilikwepa kulipa kodi na kwamba ilikuwa mbioni kubadili jina kwa lengo la kukwepa kodi.

Akitoa ufafanuzi, Mkurugenzi wa Masoko na Bidhaa wa hotel hiyo, Seraphine Lusala alisema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote na kwamba hotel hiyo imefunga sehemu ndogo ya lango lake kupisha ukarabati unaendelea.

Lusala alimwambia wana habari jana kuwa huduma zinaendelea kutolewa na wana habari walishuhudia wageni wakiingia kupitia mlango mwingine.

Alisema zoezi la kufanya ukarabati katika sehemu mbalimbali hotelini hapo litachukua takribani miezi nane kukamilika.

 

Yemi Alade Adai Alifanya Shows 300 bure
Ujerumani yammwagia Sifa Magufuli