Ufaransa imeandaa kumbukumbuku za wiki nzima za Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kuanzia Jumapili 04.11.2018, ambapo viongozi 80 kutoka ulimwenguni kote watashiriki maadhimisho ya karne moja tangu vita hivyo vilipokamilika.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron anajiandaa kwa wiki yenye shughuli nyingi za kidiplomasia ambapo atakuwa mwenyeji wa viongozi akiwemo Rais wa Marekani, Donald Trump na mwenzake wa Urusi Vladmir Putin.

Pia atafanya ziara za Kaskazini mwa Ufaransa, akitembelea maeneo yaliyohushudia mapambano ambako mamia kwa maelfu ya wanajeshi walipoteza maisha yao kwenye mitaro.

Aidha, Macron atatumia fursa hiyo ya kimataifa kutoa onyo dhidi ya kuongezeka kwa siasa kali za umaarufu mbele ya Trump anayendeleza sera ya Marekani Kwanza na viongozi wengine wa siasa za kizalendo.

Hata hivyo, maadhimisho hayo yatafikia kilele chake katika sherehe itakayofanyika katika lango la Arc de Triomphe mjini Paris, Novemba 11 na kuhudhuriwa na viongozi kadhaa akiwemo Trump, Putin na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, miaka 100 tangu kusainiwa makubaliano ya kuweka chini silaha.

 

Video: Serikali yajitenga na kampeni ya Makonda, Wanaojinyonga idadi inatisha
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 5, 2018