Timu ya Taifa ya Ufaransa imetangazwa kuwa washindi rasmi wa Fainali za Kombe la Dunia 2018, baada ya kuichapa Croatia 4-2 katika mtanange ulioshuhudiwa jioni hii katika uwanja wa Luzhniki jijini Moscow,  nchini Urusi.

Ufaransa ilikuwa ya kwanza kupata goli baada ya Mario Mandzukic kujifunga kwa kichwa katika dakika ya 18. Croatia walijibu dakika ya 28, Ivan Perisic akisawazisha goli.

Hata hivyo, makosa yaliyofanywa na Croatia yaliwapa Ufaransa penati ambayo ilifungwa kiufundi na Antoine Griezmann akiipatia timu yake goli la pili.

Pogba alizivuruga zaidi ndoto za Croatia baada ya kupachika goli la tatu katika dakika ya 59.

Mbappe aliwahakikishia Ufaransa ushindi mnono baada ya kupachika goli la nne na la mwisho kwa timu yake katika dakika ya 65. Mario alirudisha machungu  ya kujifunga kwa kuipatia Croatia goli la pili kutokana na makosa ya golikipa aliyecheza vibaya na mpira miguuni na kufanya matokeo kuwa 4-2.

Ufaransa wameshinda Kombe la dunia kwa mara ya pili tangu walipolibeba mwaka 1998 walipokuwa wenyeji wakiibamiza Brazil 3-0.

Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Julai 16, 2018
Mkuu wa Wilaya Kahama atenguliwa, Rais Magufuli afanya uteuzi mwingine