Katika kuhakikisha kuwa wakimbizi wanapata haki zao za msingi, Serikali ya Ufaransa imetoa msaada wa Euro 250,000 kwa Shirika la Chakula Duniani WFP kwaajili ya wakimbizi walioko nchini Tanzania ili kuweza kuhakikisha kuna usalama na chakula kinapatikana kirahisi.

Msaada huo wa Ufaransa utaliwezesha Shirika hilo kuendelea na mfumo wake wa kugawa fedha kwa wakimbizi liliouanzisha tangu Desemba mwaka jana ambapo liligawa shilingi 20,000 za Kitanzania kwa kila mkimbizi ambapo wakimbizi 10,000 walipata mgao huo.

Aidha, Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, asilimia 98 ya wakimbizi wanapenda zaidi kupatiwa msaada wa fedha wakati asilimia 83 wamesema zimewasaidia katika kuimarisha matumizi ya chakula na kupata aina mbali mbali za vyakula.

”Matokeo ya mpango huu wa,msaada wa fedha umekua si njia pekee inayopendelewa na wakimbizi zaidi ya msaada wa chakula lakini pia ni njia ambayo inasaidia kukuza uchumi wao,” amesema Michael Dunford, mwakilishi wa WFP nchini Tanzania

Hata hivyo, shirika linahitaji dola za Kimarekani milioni 6.8 kwa mwezi ili liweze kuendelea na mpango huo wa kugawa fedha na chakula kwa wakimbizi hao wa kutoka nchi za Burundi na Congo DRC walioko Tanzania.

 

Video: Lissu aipongeza mahakama kwa kutenda haki
Chelsea Wanyakua Willy Caballero