Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi 2021 na kubainisha kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 8.89.

Akitangaza matokeo hayo Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema watahiniwa 907,802 waliofanya mtihani huo wamefaulu.

“Watahiniwa 907,802 kati ya 1,107,460 waliotunukiwa matokeo wamefaulu. Watahiniwa hawa wamepata alama 121 au zaidi kati ya alama 300” amesema.

Amesema kati ya hao wasichana ni 467,967 (asilimia 81.43) na wavulana ni 439,835 (82.56).

“Mwaka 2020 idadi ya watahiniwa waliofaulu ilikuwa 833,672 hivyo idadi ya watahiniwa waliofaulu mwaka 2021 imeongezeka kwa watahiniwa 74,130 sawa na asilimia 8.89 ukilinganisha mwaka 2020” amesema.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 31, 2021
Hospitali ya kibong'oto kuwa taasisi