Madudu ya kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu ndani ya shirikisho la soka duniani FIFA, yanaendelea kudhihiri kufuatia uchunguzi unaofanywa kwa lengo la kujua ni vipi maafisa wa shirikisho hilo walivyokua akijigawia tenda.

Sehemu ya uchunguzi unaendelea kufanya hivi sasa, umebaini kwamba aliyekua makamu wa raisi wa FIFA Jack Warner alijipatia kiasi cha paund million 11, baada ya kupewa tenda za haki ya matangazo ya televisheni wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 pamoja na 2014.

Imebainika kwamba Warner alijipatia tenda hiyo baada ya kukubaliana na rais Sepp Blatter, ambaye alikubali jambo hilo kufanyika kwa kuweka sahihi yake.

Televisheni ya Uswiz iitwayo SRF imethibitisha kuwepo kwa dili hilo, baada ya kuonyesha hadharani mkataba uliosainiwa na rais wa FIFA Blatter mwaka 2005 kwa kuidhinisha haki zote televisheni kwa ajili ya michezo ya fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 zilizofanyika nchini Afrika kuisni pamoja na 2014 nchini Brazil.

Mbali na tenda hiyo kubainika pia uchunguzi mwingine umethibitisha kuwepo kwa rafu za kupendeleana kwa maafisa ndani kwa ndani huku jina la Warner likiendelea kuonekana katika hatua ya haki za kuonyeshwa kwa michezo ya michezo ya umoja wa vyama vya soka ukanda wa Caribbean (CFU) ambapo alijipatia kiasi cha dola za kimerekani 600,000 sawa na paund 389,000.

Malipo hayo yanadaiwa kufanywa mwaka 2007, ambapo kiongozi huyo alikua raisi wa umoja wa vyama vya soka ukanda wa Caribbean (CFU) na alikipendelea kituo cha televisheni cha SportsMax cha nchini Jamaica kupitia kampuni iliyosajiliwa kwa jina la J & D International (JDI) ambayo imebainika ni ya kwake.

Hata hivyo uchunguzi unaendelea kufanyika lakini bado jina la Jack Warner linaendelea kuonekana na inadhaniwa si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kupendelewa kupewa haki za televishini.

Inaelezwa kwamba hata wakati wa faianli za kombe la dunia za mwaka 1998 na 2002, mzee huyo alijihusisha na masuala la mlungula wa kupenyezewa tenda ya kujihusha na haki za kuonyesha michezo ya fainali hizo.

Bondia Khan Kusaidia Wakimbizi
Inter Milan Kidume Cha Milan