Ukaguzi uliofanywa na serikali hivi karibuni kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano umebaini kuwepo ufisadi mkubwa uliopelekea serikali kupoteza zaidi ya shilingi bilioni 48.47.

Ukaguzi huo umebaini upotevu wa kiasi hicho cha fedha kutokana makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa kinyamela bila kulipiwa kodi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ameeleza kuwa serikali imebaini ufisadi huo baada ya kuzifanyia ukaguzi bandari zote kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.

 

Jeshi la polisi linawashikilia jumla ya watu saba na linaendelea kuwasaka wengine wanane kutokana na kuhusika katika ukwepaji huo wa kodi.

 

Rufaa Ya Denis Cheryshev Yapigwa Teke
Yanga Uso Kwa Macho Na Azam FC Mapinduzi CUP