Watu 80 wameripotiwa kufa ikiwa ni pamoja na watoto 18 katika shambulizi la kigaidi lililotekelezwa jana katika mji wa Nice nchini Ufaransa.

Tukio hilo limetokea baada ya mtu mmoja mwenye bunduki aliyekuwa anaendesha Lori kuvamia katika eneo lenye mkusanyiko wa watu waliokuwa wakisherehekea maadhimisho ya Bastille ambapo mafataki mengi hurushwa.

Kwamujibu wa The Guardian, mshambuliaji huyo alirusha risasi kiholela (zigzag) akilenga kuua idadi kubwa zaidi kadiri awezevyo. Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, Jean- Michel Pretre, amesema Polisi walifanikiwa kumpiga risasi na kumuua mshambuliaji huyo aliyeendesha Lori lake umbali wa kilometa 2 akitekeleza tukio hilo.

Mwanamke aliyempoteza mtoto wake wa kiume akilia pembeni ya aneo la tukio

Mwanamke aliyempoteza mtoto wake wa kiume akilia pembeni ya aneo la tukio

Rais wa Ufaransa, Francois Hollande amelitaja tukio hilo kuwa baya la kigaidi na kuahidi kuwa nchi yake itakuwa imara na itapambana na magaidi ndani na nje ya mipaka yake. Alisema tayari ameamuru jeshi kuingilia kati kuwasaidia polisi hususan katika maeneo ya mipakani.

Hollande ameitisha mkutano wa dharura jijini Paris huku hali ya hatari dhidi ya mashambulizi ya kundi la Kigaidi ya ISIS ikiendelea. Hata hivyo, hadi sasa hakuna kundi lolote lililobainisha kuhusika na tukio hilo.

Picha: Zitto Kabwe aukacha ukapela, afunga ndoa na mrembo huyu
Rais Magufuli Aungwa Mkono kwa Juhudi Zake