Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Uganda, Uganda Cranes wamesusia mazoezi katika mashindano ya kombe la Mataifa ya Afrika AFCON kwasababu ya mgogoro wa malipo,

Tukio hilo ni muendelezo wa matukio yanayoendelea kutokea katika mashindnao hayo, ambapo hivi karibuni hali kama hiyo iliwakumba wachezaji wa timu za Zimbabwe, Nigeria na Cameroon.

Timu hiyo ya taifa ya Uganda, (Uganda Cranes) iliibuka nafasi ya pili katika kundi lake na inajitayarisha kukabiliana na timu ya taifa ya Senegal katika hatua ya 16 bora Ijumaa ya wiki hii.

Kwa upande wake shirikisho la mpira wa miguu nchini Uganda, FUFA limesema kuwa wachezaji hao wanajadili upya mkataba uliosainiwa kati yao na tayari limeshataja malipo ambayo yameshatolewa kwa wachezaji hao.

“Kufikia tarehe 2 Julai 2019, kila mchezaji alikuwa amepokea hadi $14,600 na marupurupu ya ziada ya kila siku na kitita cha ushindi kinachowasubiri, tunatarajia wachezaji watabadili msimamo wao   na watarudi uwanjani,” imesema taarifa hiyo iliyotolewa na FUFA

Hata hivyo, kutokana na taarifa hiyo ya shirikisho la mpira wa miguu nchini humo FUFA, wachezaji hao wa timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes) hawajatoa kauli yeyote.

Nigeria, Zimbabwe na Cameroon pia zimekabiliwa na hali kama hiyo katika kuelekea katika mashindano AFCON nchini Misri 2019.

 

 

 

Mkuu wa wilaya ya Makete asema yupo salama, amaliza kugawa Vitambulisho
Kamanda wa Polisi Arusha ajibu mapigo, 'Kaangalieni Katiba ya CCM'