Jeshi la Polisi nchini Uganda limeonya watu wanaosambaza ujumbe kwenye mitandao ya kijamii wakitishia wananchi na kuleta hofu nchini humo.

Ujumbe huo ulianza kusambazwa mwishoni mwa juma, ambapo ulitaka watu wabaki nyumbani kwa siku tatu, wakiuita ujumbe huo ‘National Shut down’.

Ujumbe huo unawaonya wananchi  wasalie nyumbani kwao bila kufanya kitu chochote kuanzia Februari 3 hadi 7.

Naibu wa jeshi la polisi nchini humo IGP Paul Oketch ametoa onyo kwa  makundi ya watu yanayosambaza vitisho hivyo kuacha mara moja kuwatisha wananchi la sivyo watachuliwa hatua kali za kisheria.

Vitisho hivi vinakuja wakati taifa hilo likiwa na mgawanyiko wa kisiasa tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa rais baada ya Rais Yoweri Museveni kutangazwa na Tume ya uchaguzi kuwa mshindi na kuongoza taifa hilo kwa muhula wa sita.

Wizara ya Kilimo yaja na huduma mpya
Joel Matip 'NDO BASI TENA'