Baada ya timu kadhaa kuaga michuano ya Afcon ambayo inafanyika nchini Misri, hatua ya mtoano inaanza leo huku  timu ya taifa ya Uganda itakua na kibarua kingine cha kukabiliana na Simba wa teranga ambao ni timu ya taifa ya Senegal.

Uganda ambao ni wawakilishi pekee kutoka Afrika Mashariki wanatazamiwa kuwa na kibarua kigumu cha kuwakabili Simba wa teranga ambao wanatizamiwa kuonesha upinzani mkali dhidi ya  Uganda The Cranes.

Mchezo baina ya Uganda na Senegal  unatarajiwa kupigwa kwenye majira ya saa moja kamili jioni katika jiji la Cairo huu mchezo mwengine baina ya Morocco na Benin utapigwa saa mbili kamili usiku.

Uimara wa Simba wa teranga ulidhihirika wakati ilipokutana na timu za Afrika Mashariki ambapo walifanikiwa kuzifunga Tanzania na Kenya katika hatua ya makundi.

Manchester United: Hatutamuongeza mshahara De Gea kama hataki basi
Serikali ya Korea yaahidi kudumisha ushirikiano na Ofisi za NBS