Serikali ya Uganda imesema kuwa itawachukua wakimbizi 2000 wa Afghanistan wanaokimbia mzozo nchini humo,kufuatia ombi la Marekani.

Hii inafuatia hatua ya wanamgambo wa Taliban kuchukua uongozi wa nchini hiyo wikendi iliyopita baada ya serikali iliyokuwa madarakani kuanguka.

Waziri wa wakimbizi Esther Anyakun amesema Rais Museveni amekubali kuwachukua jumla ya wakimbizi 2000 raia wa Afghanistan kufuatia ombi la Marekani.

Aliongeza kuwa watakapofika watafanyiwa vipimo vya corona na kuwekwa karantini. Vifaa na gharama zote zitashughulikiwa na Serikali ya Marekani.

Uganda itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwapokea watu wanaotoroka ghasia nchini Afghanistan.

Uganda ambayo imekuwa na historia ya muda mrefu ya kuwakaribisha wakimbizi kwa sasa ni nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia mzozo na majanga.

Wakimbizi nchi humo wanaoishi katika makazi au vijijini na wenyeji. Baadhi yao wamepewa kipande cha ardhi na kuruhusiwa kufnaya kazi.

Mwandishi Isah Mwandinde

Watendaji Mwanza kukiona cha Moto
Rais Samia afanya uteuzi