Idadi ya visa vya maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Uganda imefikia 274 baada ya watu wengine 10 kukutwa na maambukizi ambapo 9 ni madereva wa malori, visa hivyo vimethibitishwa baada ya sampuli 1,497 kufanyiwa vipimo.

Jumla ya madereva waliokutwa na virusi vya corona  nchini Uganda imefikia 145. Kwa mujibu wa Wizara ya Afya madereva wa malori 124 wamerudishwa nchini kwao tangu Jumamosi ya wiki iliyopita.

Hata hivyo madereva wa malori wasio na maambukizi wanaruhusiwa kuingia nchini Uganda, wale watakaopimwa na kukutwa na covid 19 hurudishwa katika nchi zao.

Young Africans kuwarudisha Eymael, Riedoh Berdien
Mganga mkuu wa mkoa ataka Dar ijikinge na Corona

Comments

comments