Idadi ya watu waliopoteza maisha katika maandamano na vurugu nchini Uganda wanaodai Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine aachiwe huru imeongezeka na kufikia 37, kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi nchini humo.

Polisi walimkamata Bobi Wine Jumatano wiki hii katika mji wa Luuka akituhumiwa kuvunja kanuni za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona kwa kufanya mkutano wa hadhara.

Tanzania: Watu nane huambukizwa VVU kila baada ya saa moja
  • Baadhi ya vijana wamechoma matairi na kufanya maandamano katika maeneo ya Jiji la Kampala na maeneo mengine wakidai mwanamuziki huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa aachiwe huru.

Polisi inawatuhumu waandamanaji kwa kufanya vurugu, kuharibu mali kama magari na kuwarushia mawe maafisa wa polisi.

Msemaji wa Polisi katika Jiji la Kampala, Patrick Onyango amesema kama hali itaendelea hivi huenda vifo vikaongezeka. Amesema watu 350 wanashikiliwa kutokana na vurugu hizo.

Sky News wamemkariri msemaji wa Jeshi la Uganda, Brigadier Flavia Byekwaso akieleza kuwa jeshi liliingilia kati kwa sababu hali ilikuwa ‘kama vita’ ambayo polisi peke yao wasingeweza kuimudu.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 21, 2020
Serengeti yang'ara Forbes