Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema Serikali imeamua kuruhusu wanafunzi wa Darasa la Sita, Kidato cha Tatu na Tano ambao wamebaki na mwaka mmoja kuhitimu masomo yao kurejea Shule kuanzia Machi 01, 2021.

Museveni amezitaka Shule na wanafunzi kuzingatia taratibu zilizopo wakati Taifa hilo likisubiri kupata Chanjo dhidi ya Covid 19 ambazo zinatarajiwa kuwasili kabla ya mwezi huu kuisha.

Rais Museveni amesema wanaweka jitihada kubwa kuzipata na wanajiandaa kuanza zoezi la utoaji Chanjo mwishoni mwa Februari au mwanzo wa mwezi Machi.

Aidha ametaja makundi yatakayopewa kipaumbele kuwa ni pamoja na watumishi wa sekta ya afya, wanaofanya kazi za usalama, walimu na wazee.

Gomez: Haikuwa rahisi
Mbunge alia na wajawazito kutozwa fedha