Serikali ya Uganda imetangaza kuwa imekubali kuwapokea wakimbizi 500 wa Eritrea na Sudan kutoka Israel na kuwahifadhi nchini humo.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Uganda anayeshughulikia masuala ya wakimbizi, Musa Ecweru alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ombi hilo liliombwa na serikali ya Israel.

Amesema kuwa zaidi ya wakimbizi 500 wamekubali kuhamishiwa nchini Uganda wakitokea Israel walikokuwa wakiishi.

Aidha, Uganda imekuwa ikisifika ulimwenguni kote kwa kuweka milango wazi kwenye sera zake za wakimbizi, kwa sasa inahifadhi wakimbizi milioni 1.4 kutoka nchi jirani.

Hata hivyo, mwanzoni mwa mwezi huu Serikali ya Israel ilibadili mawazo kuhusu makubaliano ambayo awali yalitiwa saini na shirika la wakimbizi duniani, ambapo ilikubali kutokuwaondoa wahamiaji wa Kiafrika takriban 37,000.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Aprili 14, 2018
Urusi yaiponda ripoti kuhusu shambulio la silaha za kemikali

Comments

comments