Serikali ya Uganda imempiga marufuku mbunge maarufu wa nchini Kenya, Babu Owino kukanyaga katika ardhi ya nchi hiyo kwa madai ya kuitolea lugha chafu Serikali akiwa na rafiki yake Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uganda, Haji Abubakar amemtuhumu Babu kwa kutoa maneno yasiyo ya heshima dhidi ya Serikali ya nchi hiyo hivyo atahitaji kupata kibali maalum cha wizara hiyo atakapotaka kuitembelea nchi hiyo.

“Tumebaini kazi alizofanya Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine pamoja na rafiki yake wa Kenya Babu Owino, kuishushia heshima Serikali ya Jamhuri ya Uganda iliyochaguliwa na wananchi,” alisema.

“Mtu yeyote atakayebainika kuwa amesaidia kuvunja sheria na kutoa maneno machafu dhidi ya Serikali atakabiliwa na mkono wa sheria ikiwa ni pamoja na kushtakiwa,” aliongeza Waziri huyo wa Mambo ya Ndani.

Bobi Wine ambaye ni mpinzani wa Serikali ya Uganda, alifanya mikutano kadhaa nchini Kenya ya kuzindua kampeni ya ‘Kijana kwa ajili ya Afrika’ (Youth for Africa).

Alikuwa bega kwa began a Babu Owino katika mikutano hiyo na kushiriki pamoja naye kwenye vipindi mbalimbali vya runinga.

Kutokana na mambo waliyokuwa wakiyazungumza, Serikali ya Uganda imeeleza kuwa yalikuwa yanakiuka sheria na kudhihaki utawala wa Serikali inayoongozwa na Rais Yoweri Museveni.

Steve Nyerere adai kutishiwa kuuawa
Baada ya kichapo, Mourinho anena